Skip to main content

Mafunzo maalumu yazinduliwa kuinua teknolojia ya mawasiliano

Mafunzo maalumu yazinduliwa kuinua teknolojia ya mawasiliano

Umoja wa Mataifa na Cambodia leo wamezindua mafunzo ya kusaidia uwezo wa nchi hiyo wa kutumia teknolojia ya mawasiliano kwa mipango yake ya maendeleo.

Mafunzo hayo yaitwayo Academy of ICT Essentials for Government leaders , ni miongoni mwa kozi za taasisi za umoja wa Mataifa za uchumi na kamisheni ya masuala ya jamii kwa nchi za Asia na Pasific. Mafunzo ya kwanza ya kitaifa yamehudhuriwa na maafisa 50 waunda sera , na yameanza katika hotel ya Intercontinental mjini Phnom Penh.

Mafunzo hayo ya siku nne yana lengo la kuboresha na kuinua kiwango cha matumizi ya teknolojia ya mawasiliano kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na jkijamii miongoni mwa maafisa habari na maafisa wa serikali.