Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wa Afrika wanafaidika na kuuza mazao yao nje

Wakulima wa Afrika wanafaidika na kuuza mazao yao nje

Wakulima wa Afrika wameanza kufaidika na ongezeko la watu kutaka chakula kisichorutubishwa na madawa.

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema wakulima wadogo wadogo wa afrika ya agharibi wanafaidika na ongezeko la watu wanaotaka chakula kisichorutubishwa na madawa.

Kutokana na mpango malumu wa FAO unaofadhiliwa na Ujerumani wakulima takribani 5000 kutoka nchi tano za Afrika sasa wamemudu kiwango cha mazao yako kuweza kusafirishwa kimataifa.

FAO inasema makundi ya wakulima na wasafirishaji wadogowadogo nchini Burkina Faso, Cameroon, Ghana, Senegal na Sierra Leone, walijifunza jinsi ya kuongeza utaalamu na kuimarisha uzalishaji wao, kitu ambacho kimewawezesha kupata vyeti vya kimataifa vya kusafirisha mazao yao nje.

Awali ilikuwa viogumu kwa wakulima hao kusafirisha na kuuza mazao yao nje kwa sababu hayakufikia viwango vya kimataifa.