Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu amesema amestushwa na mauaji Nigeria

Mkuu wa haki za binadamu amesema amestushwa na mauaji Nigeria

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo amesema ameshtushwa na mauaji yaliyofanyika nchini Nigeria. Amesema eneo hilo lilipaswa kulindwa vyema ili kuzuia mauaji hayo ya kikatili.

Takribani watu 200 wameuawa mwishoni mwa wiki baada ya wanaume wa Kiislamu kuvamia vijiji vinavyokaliwa na Wakristo kwenye mji wa Jos katikati mwa Nigeria. Wengi wa waliokufa wamekwishazikwa katika kaburi la pamoja.

Mkuu huyo wa haki za binadamu Navi Pillay amesema baada ya mauaji ya Januari vijiji hivyo vilipaswa kupatiwa ulinzi wa kutosha. Ameongeza kuwa wengi wa waliouawa ni wanawake, watoto na wazee.

Haya ni machafuko ya karibuni baina ya wazawa Wakristo na makundi ya wahamiaji Waislamu katika jimbo la Plateau. Na wanaochogombea mara zote ni udhibiti wa ardhi na rasilimali.