Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yaahidi nafasi zaidi za wanawake katika uongozi

Tanzania yaahidi nafasi zaidi za wanawake katika uongozi

Wakati siku ya wanawake kimataifa imeazimishwa leo kote duniani, Tanzania kuna mambo ya kujivunia na pia changamoto ambazo bado zinahitaji juhudi kufikia malengo ya Beijing ya ukombozi wa mwanamke.

Moja ya malengo makubwa ya Beijing ni kumpa fursa ya maamuzi mwanamke katika Nyanja ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Tanzania ni miongoni mwa nchi za afrika ambazo zinajitahidi kufikia malengo hayo.

Bungeni kwa sasa kuna asilimia takribani 30 ya wanawake na mwaka huu wanafanya uchaguzi mkuu ambapo serikali imeahidi kuongeza idadi ya wanawake bungeni.

Jenista Muhagama ni mbunge wa jimbo la Peramiho Songea nchini Tanzania , anahudhuria mkutano wa kimataifa wa wanawake unaotathmini mafanikio na mapungufu ya malengo ya mkutano wa kimataifa wa Beijing baada ya miaka 15. Jenista amenifahamisha mambo yakoje kwa upande wa Tanzania.