Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakosoa mfumo wa upekuzi katika viwanja vya ndege

UM wakosoa mfumo wa upekuzi katika viwanja vya ndege

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema matumizi ya mashine za upekuzi wa mwili katika viwanya vya ndege kufuatia jaribio la shambulio la kigaidi siku ya Krismas mwaka jana, ni hatua za kisiasa zaidi kuliko hatua muafa za kiusalama.

Martin Scheinin ambaye ni mwakilishi maalumu wa baraza la haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya ugaidi anasema tekinolojia ambayo inaingilia haki za watu za kujihifadhi mara nyingi hazizai matunda katika kuzuia ugaidi.

Amesema kutumia mashine ambazo zinapekua mwili mzima wa mtu kunaweza kutoa hisia zisizosahihi kuhusu masuala ya usalama na kuruhusu magaidi kutafuta mbinu nyingine kukwepa tekinolojia hiyo.