Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watalaamu wa mateso walezea yanayotendeka

Watalaamu wa mateso walezea yanayotendeka

Mwakilishi maalumu kuhusu masuala ya mateso Manfred Nowak leo ameliambia baraza la haki za binadamu katika ripoti yake kwamba mfumo wa mateso, hali isiyo ya kibinadamu katika mahabusu za polisi na kutokuwepo kwa ushirikiano wa serikali ndio yanayoendelea Equatorial Guinea.

Katika ripoti yake pia amebaini kuwa Uruguay na Jamaica kuna visa vichache vya utesaji lakini hali ya mahabusu ni mbaya sana.

Nowak amesema kwa nchi ambazo zilimwalika kama Uchina, Jordan, Indonesia, Equatorial Guinea na Kazakhstan zilimuweka katika ulinzi mkali na zimefanya majaribio kadhaa ya kumzuia kupata ukweli.

Na kubaya zaidi amesema kulikuwa ni Zimbabwe ambako hawaheshimu kabisa taratibu wala haki za binadamu.