Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimatifa ya wanwake

Leo ni siku ya kimatifa ya wanwake

Leo ni siku ya wanawake duniani, na siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake katika kila nyanja ni muhimu katika azma ya Umoja wa Mataifa kufikia malengo ya haki sawa na heshma kwa wote.

Bwana Ban ameyasema hayo katika ujumbe maalumu wa kuazimisha siku hii.Na kuongeza kuwa hadi pale wanawake na wasichana watakapokuwa huru kutoka kwa umasikini na kutotendewa haki, basi malengo yetu yote ya amani, usalama na maendeleo endelevu yatakuwa mashakani.

Shirika la kazi duniani linasema licha ya dalili za kupiga hatua miaka 15 tangu Beijing bado kuna tofauti kubwa baina ya wanawake na wanaume katika fursa za kazi na ubora wa kazi wanazofanya.