Mabomu ya ardhini ambayo hayajaripuka Afghanistan yatia hofu

5 Machi 2010

Kamati ya kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu ICRC imeelezea wasiwasi wake juu ya mabomu ya ardhini ambayo hayajaripuka na mabaki mengine ya silaha za vita nchini Afghanistan.

ICRC inasema mabomu ya ardhini yanawazuia watu kurejea makwao katika maeneo ambayo vita vimemalizika nchini humo.

Kamati hiyo pia inasema ina hofu juu ya majeraha na athari zingine zinazoweza kusababishwa na silaha na mabomu ya ardhini ambayo hayajaripuka kwa raia wa maeneo hayo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud