Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampenii kubwa ya polio imeanza katika nchi za Afrika ya Kati na Magharibi

Kampenii kubwa ya polio imeanza katika nchi za Afrika ya Kati na Magharibi

Watoto zaidi ya milioni 85 walio chini ya umri wa miaka mitano watapata chanjo ya polio katika nchi 19 za Afrika ya magharibi na Afrika ya kati kuanzia kesho Jumamosi. Chanjo hiyo inatolewa katika kampeni kabambe yenye lengo ya kuonyesha ushirikiano baina ya nchi hizo katika nia ya kutokomeza ugonjwa huo uliosumbua kwa mwaka mzima.

Nchi tisa za Afrika ya Magharibi na kati zikiwemo Burkina Fasso, Cameroon, Chad, Guinea, Liberia, Mali, Mauritania, Senegal na Sierra Leone zimeelezewa kuwa bado na mlipuko wa ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani WHO linasema baadhi ya nchi hizo hazina utaalamu na uzoefu wa kuweza kukabiliana na tatizo la polio.