Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania imepiga hatua katika ukombozi wa mwanamke

Tanzania imepiga hatua katika ukombozi wa mwanamke

Makala yetu ya wiki leo inazungumzia hatua zilizopigwa na nchi ya Tanzania katika kumkomboa mwanamke miaka 15 tangu mkutano wa Beijing wa 1995.

Wakati mkutano wa 54 wa kimataifa wa wanawake ukiendelea hapa mjini New York kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, nchi mbalimbali zimekuwa zikiwasilisha taarifa za maendeleo waliyopiga katika ukombozi wa mwanamke kwa kuzingatia maazimio ya Beijing.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoelezewa kujitahidi ,hasa katika kumpa mwanamke nafasi ya ngazi za maamuzi. Hivi sasa kuna asilimia 30 ya wanawake bungeni na mwaka huu kutafanyika uchaguzi mkuu ambapo wanategemea idadi ya wanawake itaongezeka katika uongozi.

Licha ya mafanikio waliyopiga lakini bado kuna haja ya juhudi zaidi kama alivyobaini mwandishi wa habari kutoka redio washirika wetu nchini Tanzania Benedict Komba katika makala hii. Ungana naye