Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maandalizi wa msimu wa kupanda yameanza Haiti:FAO

Maandalizi wa msimu wa kupanda yameanza Haiti:FAO

Maaandalizi ya msimu wa kipupwe wa kupanda yameanza nchini Haiti, na ni katika juhudi za muda mrefu za kuirejesha katika hali ya kawaida nchi hiyo amesema meneja wa FAO wa mpango wa dharura wa Haiti Alex Jones.

Jones amerejea makao makuu ya FAO baada ya ziara ya wiki kadhaa nchini Haiti kujionea athari za tetemeko la ardhi. Amesema mipango wanayoishughulikia kwa sasa ni vifaa na msaada wa kiufundi kwa ajili ya msimu wa kupabnda ambao utaanza karibuni. Pia amesema maandalizi kwa ajili ya kiangazi nayo yameanza ili kuhakikisha hakuna upungufu wa chakula.