Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kusaidia Waeritrea zaidi ya milioni moja 2010

UNICEF kusaidia Waeritrea zaidi ya milioni moja 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa maombi ya msaada wa karibu dola milioni 25 ili kupanua wigo wa shughuli zake nchini Eritrea.

Mashirika ya misaada yanasema Eritrea inakabiliwa na ukame ambao umesababisha upungufu wa chakula na maradhi ya utapia mlo.

UNICEF inasema itasaidia zaidi ya Waeritrea milioni moja katika mwaka huu wa 2010 ambao ni karibu robo ya watu wote wan chi hiyo, kwa kuwapa lishe bora ili kukabiliana na utapia mlo unaowazonga.

Katika ripoti yake UNICEF inasema dola milioni 13 zinahitajika, kwa sababu katika maeneo mengine asilimia 17 ya watoto wameathirika na utapia mlo.Afrika mashariki inakadiriwa watu milioni 23 wako katika hatari ya baa la njaa.