4 Machi 2010
Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekubali kutoa msaada wa dharura kwa Waganda walioachwa bila makazi kufuatia maporomoko makubwa ya ardhi mashariki mwa nchi hiyo.
Maporomoko hayo yaliyoanza siku ya Jumanne yametokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa na mafuriko yaliyosomba watu na nyumba zao hususani katika wilaya ya Bududa kilometa 275 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala. Kwa mujibu wa takwimu za awali za serikali watu 80 wameuawa na wengine 300 hawajulikani waliko.
Jopo la wafanyakazi wa UNHCR hivi sasa wako nchini Uganda kukusanya na kugawa msaada wa awali kama anavyoeleza afisa wa UNHCR mjini Nairobi Yusuf Hassan.