Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo Togo wanapiga kura kumchagua Rais

Leo Togo wanapiga kura kumchagua Rais

Wananchi wa Togo leo wanapika kura katika uchaguzi mkuu wa Rais baada kusubiri kwa muda mrefu. Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limekuwa msitari wa mbele kuhakikisha kwamba uchaguzi wa leo wa Rais ambao siku za nyuma ulighubikwa na machafuko baada ya kuzuka utata mwaka 2005 unafanyika kwa amani na kuheshimu haki za binadamu.

UNDP imeshiriki katika mradi uliogharimu mamilioni ya dola kusaidia uchaguzi huo wa Togo. Katika mradi huo UNDP imesaidia kurekebisha orodha ya wapiga kura ya mwaka 2007 na matokeo yake idadi ya wapiga kura imeongezeka kwa asilimia 11, na hivyo kuifanya idadi ya wapiga kura nchini humo kufikia karibu milioni 3.3

Na teknolojia ya biometrics imesaidia sana kuharakisha zoezi la utoaji wa kadi za wapiga kura. Zaidi ya wataalamu, wahudumu wa sensa na wakufunzi 36,000 wameajiriwa na kupelekwa kwenye vituo zaidi ya 35,000 vya kupigia kura nchini humo.