Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapendekezo ya vikwazo vipya kwa Iran yameanza kusambazwa

Mapendekezo ya vikwazo vipya kwa Iran yameanza kusambazwa

Mataifa muhimu ya magharibi na yenye nguvu yametuma mapendekezo ya vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa Urusi na Uchina. Vikwazo hivyo vitakilenga kikosi chenye nguvu nchini Iran cha wanamgambo wanamapinduzi, na kukaza uzi kwa vikwazo vilivyopo dhidi ya usafirishaji ,masuala ya bank na sekta ya bima.

Mataifa hayo pia yamewafahamisha wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa kuhusu hatua hiyo. Kwa mujibu wa balozi wa Urusi kwenye UM Vitaly Churkin baraza la usalama bado halijaanza kuyafikiria mapendekezo hayo ya vikwazo vipya dhidi ya Iran.

Balozi huyo amesema bado kuna fursa ya suluhisho la kisiasa na kidiplomasia na amekataa kutaja ni lini litapitishwa azimio la vikwazo vipya endapo mataifa hayo sita yenye nguvu yatashindwa kupata ushirikiano kutoka Tehran.