Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon ataka UM uwe mfano katika kuwapa nafasi wanawake

Ban Ki-moon ataka UM uwe mfano katika kuwapa nafasi wanawake

Akiwa katibu mkuu amehakikisha kumekuwa na wanawake wengi katika nafasi za juu za uongozi sasa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Umoja wa Mataifa. Miaka 15 tangu mkutano wa kimataifa wa wanawake wa Beijing amesema kuna hatua zimepigwa.

Ameongeza kuwa ingawa kuna mengi ya kujivunia lakini tusibweteke na kujisahau. Amesema ubaguzi na kutotendewa haki kwa wanawake kumeenea kila mahali . Hadi asilimia 70 ya wanawake wameshapitia ukatili kutoka kwa waume zao au wenza wao.

Na wakati mwingine utasikia ikisemwa kwamba hali hiyo eti ni utamaduni wa watu. Bwana Ban amesema si kweli huo sio utamaduni, bali ni unyanyasaji na wanaotenda hayo ni wahalifu na wanawanyima wanawake haki zao za msingi. Na si hayo tu bali hata ndoa za lazima, mauaji kwa misingi ya miala , ubakaji na kusafirisha watu kiharamu. Kwa kuazimisha siku ya wanawake duniani mwaka huu ambayo husherehekewa kila tarehe 8 March bwana Ban amesema ameishauri tumeinayoshughulikia masuala ya wanawake kuendeleza mambo yenye manufaa na kurekebisha ambayo bado yanamkandamiza mwananke.