Skip to main content

Mapigano yanayoendelea Darfur yaongeza hofu kwa wakimbizi wa ndani

Mapigano yanayoendelea Darfur yaongeza hofu kwa wakimbizi wa ndani

Wiki kadhaa za mapigano yanayoendelea katika baadhi ya sehemu za jimbo la Darfur Sudan yameongeza wasiwasi kwa usalama wa raia, hasa baada ya ukosefu wa usalama kuyafanya mashirika ya misaada ya kibinadamu kusitisha shughuli zake katika baadhi ya sehemu.

Mapigano hayo yamesababisha watu kuyakimbia makazi yao katika eneo la Jebel Marra katika jimbo la kusini mwa Darfur na pia jimbo la kaskazini, magharibi mwa Jebel Marra na jimbo la magharibi mwa Darfur la Jebel Moon.

Kundi la waasi lililokataa kujiunga katika mchakato wa amani ambalo linaongozwa na Abdel Wahid Nour la Sudan Liberation Army (SLA) limeyashutumu majeshi ya serikali kwa kushambulia vituo vyake mashariki mwa Jebel Marra.