ICRC imeanza kusafirisha matufaa kwenda Syria

ICRC imeanza kusafirisha matufaa kwenda Syria

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC leo imeanza kusafirisha matufaa kupitia Kuneitra kuvuka mpaka baiana ya eneo la Golan na Syria.

Hadi tani elfu kumi za matufaa zitasafirishwa katika operesheni inayotarajiwa kuchukua wiki nane.

ICRC inatumika kama mpatanishi kutokana na maombi ya wakulima wa eneo linalokaliwa na Golan na kwa idhini ya serikali ya Syria na Israel.

Kusafirishwa kwa matufaa hayo kuvuka mpaka ni moja ya safari chache zinazofanyika kutoka Golan kuingia Syria .