Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa dharura wahitajika kusaidia wanafunzi Mongolia

Msaada wa dharura wahitajika kusaidia wanafunzi Mongolia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema msaada wa haraka unahitajika kuwasaidia wanafunzi takribani 4000 katika eneo lililoathirika vibaya na msimu wa baridi nchini Mongolia.

Watoto hao ilibidi wahamishwe kwa kutumia ndege mwishoni mwa wiki, kwa ushirikiano wa UNICEF na serikali ya Mongolia. Baadhi ya vitu wanavyohitaji ni pamoja na mablanketi, viatu vinavyozuia baridi, vifaa vya usafi na vifaa vya shule kama madaftari, kalamu na vitabu.

Vifaa hivyo vitagawiwa kwa watoto waliokuwa wanaishi katika shule za bweni katika maeneo ya vijijini magharibi mwa nchi hiyo, ambako msimu wa baridi umewaathiri vibaya.