Skip to main content

WHO inasema maradhi ya kuambukiza yamepungua Haiti

WHO inasema maradhi ya kuambukiza yamepungua Haiti

Shirika la afya duniani WHO linasema tathimini yao inaonyesha kuwa hakuna ongezeko la maradhi ya kuambukiza nchini Haiti.

Linasema maambukizi katika mfumo wa hewa ndio imekuwa chanzo kikubwa cha magonjwa, ikifuatiwa na athari za hofu, majeraha, kuharisha na malaria. Shirika hilo linasema idadi ya watu wanaoshukiwa kuwa na malaria imeongezeka kutoka asilimia tano hadi kumi.

Ili kutoa huduma kwa watu wote walioathirika WHO inashirikiana na shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM, ambalo kwa sasa limeanzisha mradi mpya wa kutafuta maeneo zaidi ya 414 ndani na nje ya mji mkuu Port-au-Prince ambayo yanahifadhi waathirika wa tetemeko la ardhi laki 603,000.