Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 54 cha wanawake kimeanza New York

Kikao cha 54 cha wanawake kimeanza New York

Leo kikao cha 54 cha wanawake kimeanza hapa mjini New York Marekani. Kikao hicho kinachohudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka sehemu mbalimbali duniani na mashirika ya Umoja wa Mataifa, kitatathmini ajenda za mkutano wa Beijing uliofanyika mika 15 iliyopita.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr Asharose Migiro amesema masaula ya haki na usawa wa kijinsia bado yanapewa kipaumbe na Umoja wa Mataifa na ni jambo ambalo serikali mbalimbali zinatakiwa kuendelea kulipa kipaumbele.

Amesema hatua zimepigwa lakini kibarua bado kipo kufikia malengo yaliyowekwa Beijing na mengine yanayoendelea kujitokeza kila siku.