IAEA yaonya juu ya Iran kutotoa ushirikiano wa mipango yake ya nyuklia

IAEA yaonya juu ya Iran kutotoa ushirikiano wa mipango yake ya nyuklia

Mkuu wa shirika la kimataifa la masuala ya nyuklia IAEA Yukiya Amano amesema Iran haitoi ushirikiano wa kutosha kwa shirika la kimataifa la nguvu za atomic katika uchunguzi wake wa shughuli za nyuklia za Jamuhuri hiyo ya Kiislam.

Amesema ushirikiano unaotakiwa ni pamoja na kutekeleza maazimio ya bodi ya magavana wa AIEA na ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.