Skip to main content

Sudan na kundi la JEM wafungua ukurasa mpya wa amani

Sudan na kundi la JEM wafungua ukurasa mpya wa amani

Serikali ya Sudan na kundi la JEM mapema wiki hii waliamua kufungua ukurasa mpya walipoamua kutia saini makubaliano ya mchakato wa amani mjini Doha Qatar.

Kiongozi wa kundi hilo Khalili Ibrahim amesema makubaliano hayo ni muhimu saana katika kuelekea amani ya kudumu kwenye jimbo la Darfur.

Umoja wa Mataifa, vikosi vya kulinda amani Daurfir UNAMID, na watu mbalimbali wamepongeza hatua hiyo. Lakini je ni hatua itakayomaliza mzozo wa dafur, au ni mchezo wa kila siku wa paka na panya? Kujadili hatua hiyo na matarajio ya amani ya kudumu Sudan nimezungumza na Dr Salim Ahmed Salim aliyekuwa mwakilizi wa Umoja wa Afrika katika upatanishi wa mzozo huo wa Darfur, kwanza ameionaje hatua hiyo?