Msaada wa Kimataifa unahitajika kuisaidia Haiti kupambana na Ukimwi

Msaada wa Kimataifa unahitajika kuisaidia Haiti kupambana na Ukimwi

Haiti ambayo imesambaratishwa na tetemeko la ardhi la Januari 12 inahitaji kuwezeshwa ili kuanza tena shughuli ya kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya Ukimwi. Baada ya UNAIDS na wizara ya afya na idadi ya watu ya Haiti kutathimin hali halisi, UNAIDS imetoa ripoti iitwayo "kuisaidia Haiti kurejesha uwezo wake wa kupambana na Ukimwi".

Ripoto hiyo inaelezea hali ya sasa ya ukimwi Haiti na nini mahitaji ya haraka na ya muda mrefu ya kukabiliana na tatizo la Ukimwi.

Nalo shirika la OCHA linasema wakati Port-au-Prince mahitaji ya muhimu kama chakula, maji ya kunywa na huduma za afya vinapatikana, mashirika ya misaada yanayofanya kazi katika miji ya jirani wanaendelea kukabiliana na kazi ya kuwasaidia watu binafsi na pia jamii mbalimbali aambao wanahitaji maji, chakula, malazi na madawa.