Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wa Mazingira wasisitiza juhudi zaidi kukabiliania na uharibifu

Mawaziri wa Mazingira wasisitiza juhudi zaidi kukabiliania na uharibifu

Mawaziri wa mazingira kutoka kote duniani wametoa azimio lao la kwanza baada ya muongo mmoja. Katika azimio hilo serikali zao zimeahidi kuongeza juhudi za kimataifa ili kukabiliana na changamoto kubwa za mazingira na zinazorudisha nyuma maendeleo.

Azimio hilo limeelezea umuhimu wa viumbe hai, umuhimu wa haraka wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kufanya kazi pamoja ili kupata matokeo mazuri katika mkutano utakaofanyika Mexico baadaye mwaka huu. Pia limebaini fursa ya kuwa na matumizi madogo ya gesi ya cabon na kuchagiza maendeleo ya uchumi unaolinda mazingira.