Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamekosoa wito wa Libya wa Jihad dhidi ya Switzerland

26 Februari 2010

Leo Umoja wa Mataifa umeamua kuunga mkono upande wa Switzerland baada ya kiongozi wa Libya Moamar Gadaffi kutoa wito wa kuendesha vita vya Jihad dhidi ya Switzerland.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema wito wa kiongozi huyo wa Libya ni kitendo kisichokubalika. Alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu taifa moja kutangaza vita vitakatifu dhidi ya taifa lingine, mkurugenzi mkuu wa Umoja wa Mataifa Seigei Ordzhonikidze amesema, anaamini katika masuala ya uhusiano wa kimataifa kiongozi wa nchi kutangaza jambo kama hilo ni kinyume na taratibu za kimataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter