Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya tumbaku yanaongezeka katika nchi zinazoendelea: WHO

Matumizi ya tumbaku yanaongezeka katika nchi zinazoendelea: WHO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani Margaret Chan ameonya kwamba matumizi ya tumbaku yanaongezeka sana katika nchi zinazoendelea.

Bi Chan amesema kama matumizi ya tumbaku yanapungua katika baadhi ya sehemu duniani basi yanaongezeka katika maeneo mengine. Ameyasema hayo katika maazimisho ya mwaka wa tano tangu mkataba WHO wa kudhibiti matumizi ya tumbaku kuanza kufanya kazi.

Amesema ni lazima kukiri kwamba matokeo mazuri yanahitajika, na leo amesema ndio siku muafaka ya kufikiria mkataba huo ulimaanisha nini ulipoanza kutekelezwa miaka mitano iliyopita na ahadi zake kwa siku za usoni. Hata hivyo amekiri kuwa katika baadhi ya nchi kiwangio cha matumizi ya tumbaku kimepungua.

Na ameongeza kuwa kupungua huko kumesaidia kupunguza visa vya magonjwa ya moyo, kiharusi, saratani na magonjwa mengine yanayohusishwa na matumizi ya tumbaku. Lakini amesema hata hivyo katika nchi hizo matumizi ya tumbaku bado ni ya kiwango cha juu hususani kwa watu wa kipato cha chini.