Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano ya kikabila yameshika kasi Sudan Kusini

Mapigano ya kikabila yameshika kasi Sudan Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya msaada wa kibinadamu OCHA linasema mapigano ya kikabila yameongezeka sana Sudan Kusini tangu mwezi Desemba 2009 na kuendelea hadi Januari na Februari mwaka huu wa 2010.

OCHA inasema zaidi ya visa 39 vya mapigano ya kikabila vieripotiwa Sudan Kusini na vimesababisha vifo vya watu 541, na wengine 34,139 wameachwa bila makao kutokana na machafuko hayo. Kama anavyofafanua msemaji wa OCHA