Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Botswana yatakiwa kushughulikia matatizo ya jamii za kiasili

Botswana yatakiwa kushughulikia matatizo ya jamii za kiasili

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binadamu na uhuru wa watu wa jamii za kiasili, Prosefa S James Anaya leo ameitaka serikali ya Botswana kushughulikia kikamilifu masuala yanayozikabili jamii nyingi za watu asili (indigineous people).

Akizindua ripoti yake kuhusu matatizo ya jamii hizo nchini Botswana bwana Anaya amesema jamii hizo zinakabiliwa na masuala matatu makubwa. Kwanza ni wao kutambulika na utamaduni wao kuheshimiwa , pili kushiriki katika masuala ya siasa na kuulizwa mawazo yao na mwisho ni kujaribu kufuta yale makosa ya kihistoria.

Katika ripoti yake aliyoiandaa baada ya ziara yake nchini humo mwezi March 2009 Profesa Anaya amesifia baadhi ya hatua zilizochukuliwa na serikali kuangalia maslahi ya jamii hizo lakini amesema juhudi zaidi ziongezwe ili kutatua masuala muhimu yanayozisumbua jamii hizo.