Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nigeria yatakiwa kupambana na maambukizi ya HIV kutoka kwa mama hadi kwa mtoto

Nigeria yatakiwa kupambana na maambukizi ya HIV kutoka kwa mama hadi kwa mtoto

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya ukimwi UNAIDS Michel Sidibe yuko ziarani nchini Nigeria.

Akiwa nchini humo bwana Sidibe amesema Nigeria ni lazima iwe msitari wa mbele katika kutekeleza ajenda ya kikanda na ya Umoja wa Afrika ya kutokemeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ifikapo mwaka 2015.

Amesema bila Nigeria kushika usukani, lengo hilo halitofikiwa barani Afrika. Kuna takribani watu milioni tatu wanaoishi na virusi vya HIV nchini Nigeria. Ukiacha Afrika ya Kusini Nigeria ndio inayofuatia kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi vya HIV barani Afrika.

Kila siku kuna maambukizi mapya 1000 na kiwango cha taifa cha maambukizi ni karibu asilimia 4.6%.