Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICTR yamfunga miaka 25 mkuu wa zamani wa sheria wa Rwanda

Mahakama ya ICTR yamfunga miaka 25 mkuu wa zamani wa sheria wa Rwanda

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 ICTR iliyoko mjini Arusha Tanzania, leo imemuhukumu kwenda jela miaka 25 Luten Kanali Ephrem Setako.

Bwana Setako alikuwa mkuu wa masuala ya sheria katika wizara ya ulinzi ya Rwanda mwaka 1994. Mwandishi wa habari za kesi za mauaji hayo mjini Arusha Tanzania Nicodemus Ikonko anaarifu.