Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea ziko katika hatari ya ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Nchi zinazoendelea ziko katika hatari ya ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza

Mkuu wa shirika la aya duniani WHO Margaret Chan ameonya kuwa kuna tatizo la magonjwa yasiyo ya kambukiza na tatizo lenyewe ni kubwa na huenda likaongezeka.

Bi Chan ameuambia mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mjini Geneva kwamba , magonjwa hayo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakichukuliwa kuwa ni ya watu wa nchi zilizoendelea , sasa yamebadili mwelekeo.

Magonjwa kama ya moyo, saratani, kisukari, magonjwa ya kushindwa kupumua na upungufu wa akili, sasa yamekuwa mzigo mkubwa kwa nchi za kipato cha wastani na zile za kipato cha chini.

Magonjwa ambayo yalikuwa yanachukuliwa kuwa ni ya matajiri sasa yanawaandama msikini na wasio jiweza amesema Bi Chan. Nchi hizo zimekumbwa na maradhi hayo na hazina uwezo wa kuyakabili.