UNAMID yapongeza makubaliano ya amani ya serikali ya Sudan na kundi la JEM

24 Februari 2010

Mpangu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan umepongeza hatua ya maafikiano ya kumaliza mzozo wa Darfur baiana ya serikali ya Sudan na kundi la Justice and Equality movement JEM, yaliyotiwa saini mjini Doha Qatar.

Mwakilishi wa UNAMID Ibrahim Gambari ambaye alikuwepo Doha kushuhudia hafla ya kutia saini makubaliano amezipongeza pande zote husika kwa juhudi zao.

Ameongeza kuwa UNAMID inasubiri kwa hamu utekelezaji wa mkataba huo na ameyataka makundi mengine ya waasi kufuata nyao. Kemal Saiki mkuu wa mawasiliano wa UNAMID amesistiza kuwa vita haimalizwi kwa mtutu wa bunduki na hatua ya suluhu waliyofikia ni muhimu sana katika kuisaidia jamii ya Darfur.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter