Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la JEM Darfur lasaini mkataba wa amani

Kundi la JEM Darfur lasaini mkataba wa amani

Kundi la waasi lenye ushawishi mkubwa kwenye jimbo la Darfur na serikali ya Sudan wametia saini makubaliano ambayo yatafungua njia ya majadiliano ya kisiasa ili kumaliza miaka saba ya mvutano.

Kiongozi wa kundi hilo la Justice and Equality Movement (JEM) Khalil Ibrahim amesema makubaliano hayo ya kusitisha vita yanaanza kutekelewa usiku wa leo. Umoja wa Mataifa unakadiria watu laki mbili wameuawa katika vita baiana ya pande hizo mbili.

Ibrahim ameyaatia makubaliano hayo kama hatua muhimu, lakini ameonya njia ya kuelekea amani inahitaji uvumilivu na masikizano kutoka pande zote. Kuimarika kwa uhusiano baina ya Sudan na Chad ambapo siku za nyuma kila mmoja alikuwa akimlaumu mwenzake kwa kusaidia makundi ya waasi, umesaidia kuafikiwa kwa mkataba huo.

Makubaliano hayo yametiwa saini katika hafla iliyofanyika mjini Doha Qatar na mwenyeji wa sherehe hizo kiongozi wa Qatar amesema zitakusanywa dola bilioni 1.5 kwa ajili ya maendeleo ya Darfur.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Marekani, Umoja wa Mataifa, wawakilishi kutoka nchi za Kiarabu na Rais wa Chad.