Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP inasema juhudi zaidi zahitajika kupunguza gesi za viwandani

UNEP inasema juhudi zaidi zahitajika kupunguza gesi za viwandani

Mpango wa Umoja wa Mataifa unaohusika na Mazingira UNEP umesema nchi zote duniani lazima ziwe na hamasa ya ziada katika kupunguza kiwango cha gesi ya viwandani, endapo dunia inataka kweli kukabiliana na ongezeko la joto, na kulipunguza hadi nyuzi joto 2 au chini ya hapo.

Utafiti huo mpya uliozinduliwa na baraza linalosimamia UNEP kwenye kongomano la mazingira linalofanyika mjini Bali Indonesia, limetanabaisha pia ahadi zilizotolewa na nchi 60 zilizoendelea na zinazoendelea.