Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaadhinisha mkopo kuisaidia Yemen

UNHCR yaadhinisha mkopo kuisaidia Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo linakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha katika shughuli zake nchini Yemen, limeidhinisha mkopo wa ndani wa dola milioni 4.7, ili keundelea na shughuli zake za kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini humo hadi katikati ya mwaka huu.

Hatua hii ni ya kuepuka kusitisha au kufunga programu zake Yemen, hatua ambayo ingekuwa na athari kubwa na hususani kwa raia ambao walilazimika kuwa wakimbizi wa ndani kufuatia mapigano ya miezi saba baiana ya serikali na vuguvugu la Al Houti kaskazini mwa Yemen. UNHCR inasema mchango mdogo wa wafadhili mwaka huu unatishia shughuli zake za juhudi za kuwalinda raia na kutayarisha orodha ya wakimbizi wa ndani, pia kusaidia mahitaji ya wakimbizi hao hasa watoto, wanawake na wazee.