Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpatanishi wa mgogoro wa Ivory Coast asema suluhu iko karibu

Mpatanishi wa mgogoro wa Ivory Coast asema suluhu iko karibu

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory coast Y J Choi amekutana na mpatanishi wa mgogoro wa nchi hiyo Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso katika jitihada za kutatua mgogoro huo wa kisiasa.

Baada ya mkutano wao mpatanishi Rais Compaore, mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa alifanya mkutano na waandishi wa habari na kusistiza kwamba  mgogoro huo lazima utatuliwe.

Naye mpatanishi Rais Copaore wa Burkina Faso amesema baada ya kujadiliana na pande zote husika ameona kuna matumaini makubwa ya suluhu na hatua imepigwa katika kuifikia.