Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kutumia teknolojia kuendeleza kilimo

FAO kutumia teknolojia kuendeleza kilimo

Mkutano kiufundi wa kimataifa wa FAO kuhusu masuala ya tekinolojia ya kilimo katika nchi zinazoendelea umeanza.

Nchi zinazoendelea hivi sasa zinakabiliwa na ongezeko la matatizo makubwa ya upungufu wa chakula , matatizo yanayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa . Matatizo haya yatachangoa hali ya maisha kwa mamilioni ya watu kuwa mbaya zaidi.

Mkutano huo utajadili ni kwa vipi tekinolojia ya kilimo itachangia kuzisaidia nchi zinazoendelea. Mkutano huo pia utadadisi fursa zilizopo na ushirikiano ili kuimarisha uwezo wan chi zinazoendelea kuchagua na kutumia tekinolojia muafaka.

Mkutano huo utagusia Nyanja zote za teknolojia ya kilimo ikiwa ni pamoja na vyakula vyote, sekta zote za kilimo kama mazao, uhifadhi wa misitu, mifugo, uvuvi na zana za kilimo.

FAO unasisitiza kwamba ni muhimu tekinolojia ikatumiaka pia kutatua shida za wakulima wadogowadogo , wavuvi na wanaotegemea misitu katika nchi zinazoendelea ili kukabiliana na matatizo ya upungufu wa chakula na mabadiliko ya hali ya hewa.

Tekinolojia hiyo ya kilimo inaweza kutumika katika matumizi mbalimbali kama kuboresha aina za mazao kwa upandikizaji, kwa wanyama kwa kuongeza uzalishaji wa mazao yao, kutunza misitu, kuhifadhi chakula , kugundua magonjwa na mimea na wanyama , kutengeneza chanjo na kuimarisha malisho.