Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wakutana kujadili jinsi msaada, madeni na uwekezaji unavyoweza kuzisaidia nchi zinazoendelea

Wataalamu wakutana kujadili jinsi msaada, madeni na uwekezaji unavyoweza kuzisaidia nchi zinazoendelea

Wataalamu 18 wanakutana katika makao makuu ya UNCTAD kwa siku nne zijazo ili kuepeleleza, jinsi nchi zinazoendelea zitakavyoweza kusaidiwa kuimarisha uwezo wake wa uzalishaji.

Mkutano huo waliouita "mchango na matumizi mazuri ya msaada wa nje kwa maendeleo hususani katika kuandaa uwezo wa uzalishaji" umeamua kuchukua mtazamo huo hasa wakati huu ambapo nchi masikini zikisuasua kukabiliana na athari za mtikisiko wa kiuchumi ulioikumba dunia.

Mkutano huo utazingatia zaidi jinsi uwezo wa uzalishaji utakavyoweza kuimarishwa kwa kupitia sera za maendeleo ya uchumi, msaada wa maendeleo, madeni ya nje na uwekezaji .