Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za haraka zahitajika kuziandaa nchi zinazoendelea na taka za vifaa vya umeme

Hatua za haraka zahitajika kuziandaa nchi zinazoendelea na taka za vifaa vya umeme

Ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mastaifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP, inasema taka za vifaa vya umeme inaongezeka duniani na imefikia tani milioni 40 kwa mwaka.

Ripoti hiyo inasema kama hakutachukuliwa hatua za haraka za kukusanya na kuzitokomeza taka hizo basi nchi nyingi zinazoendelea zitakabiliwa na hatari ya mrundikano wa taka hizo kama computa na simu za mkononi , ambazo zinaweza kusababisha athari kubwa kwa afya na mazingira. Imeongeza kuwa uuzaji wa vifaa vya umeme katika nchi kama Uchina na India kwenye mabara mengine ikiwemo Afrika na Amerika ya Kusini kutaongezeka saana katika miaka kumi ijayo. Na kama anavyosema Guido Sonneman wa UNEP baada ya matumizi ndipo palipo na shida.

(CLIP E-WASTE GUIDO)