Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na Sudan kufanyia mabadiliko mfumo wa magereza Sudan

UM na Sudan kufanyia mabadiliko mfumo wa magereza Sudan

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na ule wa Afrika kwenye jimbo la Darfur, kwa kushirikiana na serikali ya Sudan wametia saini makubaliano ya kuimarisha mfumo wa magereza na hali ya wafungwa nchini Sudan.

Maafikiano hayo yalisainiwa kwenye mji wa El Fasher kaskazini mwa Darfur, ambako ndio makao makuu ya mpango huo wa kulinda amani ujulikanao kama UNAMID.

Lengo la mkataba huo ni kuimarisha ushirikiano baiana ya UNAMID na serikali ya Sudan katika maeneo kama ya kutoa mafinzo kwa maafisa wa magereza, kuboresha hali ya magereza na kuchagiza programu za kubadili tabia kwa wafungwa, kama anavyoeleza mkurugenzi wa UNAMID Germain Baricako.