Mkutano wa Kimataifa wafanyika kujadili huduma na matokeo ya hali ya hewa
Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa linalohusika na utabiri wa hali ya hewa, Michel Jarraud amesema changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ni dhahiri na zinagusa nyanja zote za kijamii, kiuchumia na sekta ya mazingira.
Ametoa kauli hiyo mbele ya wataalamu 150 kutoka kote duniani wanaoshiriki kikao cha 15 cha tume ya hali ya hewa ya shirika hilo kinachojadili hatua za kuchukua kuimarisha huduma za hali ya hewa kwa jamii ya kimataifa. Hii inajumuisha kuanzisha jopo la wataalamu ambao watajikita katika kuangalia na kutathmini matokeo ya hali ya hewa, athari na jinsi ya kukabiliana na athari hizo.