Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa na MTV waendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI Kenya

Umoja wa Mataifa na MTV waendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI Kenya

Makala yetu ya wiki leo inamulika jitihada za Umoja wa mataifa na kituo cha televisheni cha MTV kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi nchini Kenya kwa kutumia tamthilia ya televisheni.

Umoja wa Mataifa na MTV wako katika mkakati wa kuwafikia vijana nchini Kenya na kuwaelimisha kuwa Virusi vya Ukimwi sio hukumu ya kifo kwa kutumia tamthilia mpya ya televisheni yenye sehemu tatu inagusia maisha na mapenzi ya kundi la marafiki mjini Nairobi.