Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi ujao Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kipimo cha amani na demokrasia

Uchaguzi ujao Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kipimo cha amani na demokrasia

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya haki za bindamu Navi Pillay amesema uendeshaji wa uchaguzi mkuu ujao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, utakuwa ni mtihani muhimu kwa juhudi za nchi hiyo za kuleta amani na demokrasia.

Amesema kwamba vitendo vinavyoendelea vya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu vimekuwa ni moja ya changamoto kubwa na ya muda mrefu inayoikabili nchi hiyo. Ameongeza kuwa kuimarisha mfumo wa haki na utawala wa sheria, kuondoa tabia ya ukiukaji serikalini, ikiwemo kwenye jeshi na polisi na kuacha ghasia na ukandamizaji ni vitu muhimu katika hatma ya nchi hiyo.