Skip to main content

IAEA imeelezea hofu yake juu ya mipango ya nyuklia ya Iran

IAEA imeelezea hofu yake juu ya mipango ya nyuklia ya Iran

Kwa mara ya kwanza shirika la Umoja wa Mataifa linaloangalia masuala ya nyuklia limeelezea waswasi wake kwamba Iran inajaribu kutengeneza bomu la nyuklia.

Shirika hilo pia limesema bado halijapata majibu ya masuala ya nyaraka zinazosema kwamba Iran inajihusisha katika majaribio ya mipango ya nyuklia. Hivyo inazusha maswali mengi ya uwezekano wa Iran siku za nyuma au sasa inamipango ya siri ya kuunda silaha za nyuklia.