Skip to main content

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wake wameelezea mipango yao kwa nchi ya Haiti

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wake wameelezea mipango yao kwa nchi ya Haiti

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wake wamekuwa wakielezea mipango waliyonayo katika kuendelea kuisaidia Haiti.

Shirika la umoja wa Maifa la kuhudumia watoto UNICEF linaliangalia upya ombi lake la msaada wa dola milioni 172 ili kusaidia masuala ya maji na usafi.

Shirika la Afya Duniani, WHO kwa upande wake limeongeza kiwango cha ombi la msaada na kufikia dola milioni 134 ambapo WHO na PAHO wanatarajia kukusanya dola milioni 350.

Nao Mpango wa Chakula Duniani, WFP unasema wiki ijayo utaanza kugawa chakula ambacho kimepikwa kwa watoto wa takribani shule 19. Lengo ni kuzifikia shule 50 zenye watoto wapatao laki tano.