Majaji wa ICC wanataka ufafanuzi na maelezo zaidi kuhusu hali nchini Kenya

Majaji wa ICC wanataka ufafanuzi na maelezo zaidi kuhusu hali nchini Kenya

Majaji katika kitengo cha kesi cha mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mjini The Hague Uholanzi, wamewataka waendesha mashitaka kutoa ufafanuzi na maelezo ya zaidi ,katika kutathimini hali nchini Kenya.

Maelezo hayo yanayotakiwa kutolewa kabla ya tarehe 3 Machi mwaka huu ni ya kuangalia endapo idhini itolewe au la kwa waendesha mashitaka kuanza uchuinguzi kuhusu hali ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa sheria namba 50 kifungu cha nne ya taratibu na ushahidi, kitengo cha kesi kinaweza kuomba taarifa zaidi kutoka kwa mwendesha mashitaka kama kinafikiria ni sawa ili kiweze kutekeleza wajibu wake.

Tarehe 26 Novemba 2009 waendesha mashitaka walitaka idhini kutoka kwa kitengo cha kesi ili waanze uchunguzi dhidi ya uhalifu uliotendeka Kenya wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu 2007-2008. Wanadai kuwa makosa yaliyotendeka yanajumuisha uhalifu dhidi ya ubinadamu.