Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango mpya wahitajika kuzisaidia nchi masikini kuendelea kiuchumi:

Mpango mpya wahitajika kuzisaidia nchi masikini kuendelea kiuchumi:

Wazungumzaji katika mkutano wa siku mbili wa wataalamu unaojadili changamoto za maendeleo zinazozikabili nchi masikini, wamesema mtazamo mpya ni lazima kama nchi masikini kabisa duniani ambazo hivi karibuni zimekumbwa na matatizo ya chakula na nishati, mtikisiko wa kiuchumi, na katika maeneo mengine majanga ya kiasili, zitataka kuepukana na matatizo haya.

Katibu Mkuu wa UNICTAD Supachai Panichpakdi amesema uzoefu unaonyesha kwamba nguvu za nje za kuzisaidia nchi masikini ni lazima zizingatie zaidi kuziwezesha nchi hizo kuwa na wigo mpana wa kiuchumi, wapunguze hali tegemezi katika mali ghafi au bidhaa za kilimo, mfano katika shaba, kakao na kahawa