Chad inataka vikosi vya UM vya kulinda amani viondoke

18 Februari 2010

Kiongozi wa ngazi za juu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa anakwenda nchini Chad wiki ijayo baada nchi hiyo ya Afrika kusema inataka vikosi vyote vya Umoja wa Mataifa viondoke.

Vikosi hivyo vilipelekwa nchini humo zaidi ya miaka miwili iliyopita baada ya kuongezeka mvutano katika eneo la mpakani na jimbo la Darfur la Sudan.

Ziara ya mkuu huyo wa operesheni za kulinda amani imetangazwa baada ya leo mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa nchini Chad Ahmad Allam kuuambia mkutano wa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New york, kwamba mpango huo wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad unaojulikana kama MINURCAT umeshatimiza wajibu wake.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter