Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji wahitajika haraka kunusuru sekta ya ufugaji:FAO

Uwekezaji wahitajika haraka kunusuru sekta ya ufugaji:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema uwekezaji wa haraka, juhudi za utafiti wa kilimo na utawala bora vinahitajika ili kuhakikisha sekta ya mifugo duniani inaweza kukidhi mahitaji ya mazao yatokanayo na wanyama

Na wakati huohuo sekta hiyo kuchangia kupunguza umasikini, kuhakikisha usalama wa chakula upo, kulinda mazingira na afya za watu.

Mkurugenzi wa FAO Generali Jacques Diof anasema, haya yakizingatiwa sekta ya mifugo itakuwa mchango mkubwa wa kukabiliana na matatizo mengi.